Mbunge wa jimbo la Momba Condester Michael Sichalwe ameitaka wizara ya Viwanda na Biashara kutoa taarifa ya mapato yanayotokana na vinywaji vikali inavyotoka nje ya Tanzania.
Sichwalwe ameomba hilo wakati akichangia makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameiomba SIDO na Wizara ya Viwanda kuwawezesha watanzania wenye uwezo wa kutengeneza vinywaji hivyo kwa kuwanunuliwa mitambo ya kuchakata mitambo hiyo.
“Kama vinywaji vingine vikali vinaweza kuruhusiwa kuingia nchini kwetu na watumiaji ni watanzania hawa hawa ambao wanaendelea kutumia vinywaji hivyo vikali shida iko wapi watanzania hawa kwa uwezo ambao wamepewa na Mungu wanaweza wakabuni na kutengeneza vinywaji hivyo vikali na badala ya SIDO na Wizara ya Viwanda kuwasaidia kuwatafutia mtambo wa kutofautisha Ethanol na Methanol ili tuweze kupata vinywaji vikali lakini Wizara ya Viwanda na Biashara hili jambo wameshindwa lakini wapo tayari kuendelea kuruhusu vinywaji vikali viendelee kuja nchini”.