Dodoma. Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) nchini Tanzania, Esther Matiko ametaka mkataba wa kampuni ya Star Media na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuvunjwa kwa sababu umekuwa ukijiendesha kwa hasara tangu ulipoingiwa mwaka 2009.
Esther aliyasema hayo jana Alhamisi Januari 30, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati ya Bajeti na ile ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC).
Esther alisema kampuni hiyo ilianza na mtaji wa Sh547 bilioni walisema ikifika 2014 wangeweza kutoa gawio lakini kinyume chake inajiendesha kwa hasara.
Alisema mwaka wa fedha 2014/15 walipata hasara ya Sh6.8 bilioni na kwamba cha kushangaza mtaji mwaka 2018 ni hasi ya Sh119 bilioni.
Hata hivyo, alisema Serikali ya Tanzania bado inaendelea kulikumbatia shirika hilo kama mbia na kwamba cha kushangaza hata ukitaka kuunda kamati teule kufuatilia unazuiliwa.
“Tunataka kujua kuna nini nyuma ya Star Media. Fedha za Watanzania asilimia 35 zimewekezwa pale kama wabia, tunataka kujua ni kwa nini mkataba huu usisitishwe, naomba muuvunje huu mkataba,” alisema.
Pia Soma
- Rugemarila ashangaa kushtakiwa, ahoji barua yake kwenda TRA
- Waziri wa zamani amvaa Zitto mkopo wa WB, Spika Ndugai amshangaa
- WHO yaitangaza corona janga la dunia
“Madudu ya jinai tumewakilisha kwa vyombo husika vya Serikali, ya kiutendaji tumeyafanyia marekebisho, kwa mara ya kwanza Star Media imeweza kuchangia Sh500 milioni mfuko mkuu Hazina,” alisema Dk Mwakyembe.
Alisema pia Star Media imekubali upungufu uliosababishwa na baadhi ya watendaji wake watailipa TBC Sh3 bilioni kuanzia Machi 2020.
Alisema mambo yanaenda vizuri na kwamba maelezo zaidi atayatoa katika siku za usoni.