Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Chadema ataka Bunge kujitafakari

56559 Mbungepic

Fri, 10 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Salome Makamba amesema ipo haja ya Bunge kujitafakari sababu za kutoa mamlaka ya usimamizi wa ndege kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwenda ofisi ya Rais ambayo haikaguliwi na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Makamba ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 8, 2019, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Amesema Rais John Magufuli amefanya vizuri katika kusimamia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na  amehamishia mamlaka ya usimamizi wa ndege zote za Serikali katika ofisi yake na kwamba mradi wa ununuzi wa ndege ni miongoni mwa miradi mikubwa mitatu nchini.

“Ofisi hii haikaguliwi na pesa za wananchi ambazo ndio nyingi zinatumika katika mradi huu zimehamishiwa ofisi ya Rais ambayo haikaguliwi na mkaguzi,” amesema.

Amesema kama kuna sehemu ambayo inaonyesha hasara kubwa ni katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

“Ipo haja ya kuangalia suala hili. Wakati mwingine  tunaweza kutukanisha Bunge letu bila kujua. Katika kuhamisha mamlaka anayenunua ndege ni ofisi ya Rais, akinunua nzima mbovu ni juu yake.”

 “Huyo huyo ndiye anapitisha matengenezo ya ndege, haijulikani kama amenunua mbovu ama nzima. Hata yeye ndiye ananunua mafuta ya ndege bila kujali fuel consumption (matumizi ya mafuta) kama ilizingatiwa wakati wa manunuzi,” amesema Salome.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz