Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Chadema asema yupo tayari kuacha ubunge

16031 Mbunge+pic TanzaniaWeb

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mbunge wa Serengeti (Chadema) Marwa Ryoba amesema yupo tayari kuacha ubunge ili awape wananchi waliomchagua barabara ya lami.

Akizungumza leo Septemba 6, 2018 katika ziara ya Rais John Magufuli wilayani Serengeti,  Ryoba amesema wilaya hiyo haijanufaika na Hifadhi ya Serengeti kutokana na kukosekana kwa barabara ya lami.

Amesema ingawa yupo Chadema lakini anampenda Rais Magufuli.

Mbunge huyo amemshukia mkurugenzi wa mji wa Serengeti, Juma Hamsini akidai kuwa amefuja zaidi ya Sh500 milioni.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imetenga Sh 11.2 bilioni ili kutatua tatizo la maji Mugumu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz