Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Chadema amkumbuka Mengi kwa kumpa moyo wa kutimiza ndoto zake

55284 PENEZA+PIC

Fri, 3 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge Viti Maalum (Chadema), Pendo Peneza amesema mwenyekiti mtendaji wa  IPP, Regnald Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo atamkumbuka kwa kumpa moyo wa kusonga mbele kutimiza ndoto zake za kuwa kiongozi.

Akizungumza jana Alhamisi Mei 2,2019 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Peneza alisema anakumbuka mwaka 2014 akiwa anazungumza katika kipindi cha ITV, Mengi alimuona na kuandika ujumbe mfupi katika twitter ukionyesha kufurahia namna alivyokuwa akijieleza kama mgombea uwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema.

“Aka-twitt akasema namuangalia Upendo Peneza ni kijana ambaye kutokana na jinsi anavyojieleza namuona ni shujaa wangu mdogo,” alisema.

Alisema baadaye alimpigia simu ya kumpa moyo kufikia hadi ambapo anapotaka kufika, jambo ambalo lilimsaidia katika kampeni zake za kuwania nafasi hiyo.

 “Natambua juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Mzee Mengi za kuwasaidia watu mbalimbali,” alisema.

Alisema anakumbuka kuwa Mengi alianzisha mashindano ya wazo bora la biashara kwa vijana na watu waliokuwa wakishinda walipewa fedha kwa ajili ya kuendeleza mawazo yao.

“Hii ilikuwa ni njia ya kutaka kuwanyanyua vijana mbalimbali kiuchumi. Mara ya kwanza pia alikuwa akitoa chakula kwa watu wenye ulemavu lakini baadaye alisogea na kuanza kutoa tuzo,” alisema.

Alisema hilo ni jambo zuri ambalo liliifundisha jamii kuwa ulemavu sio sababu ya kutokuwa na ndoto za mafanikio.

“Tuzo hizo zimesaidia hata kuwabadilisha wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutamani kuwapeleka shule na kuwaendeleza katika vitu wenye uwezo navyo na hatimaye waweze kujitegemea,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz