Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Chadema adai bila haki hakuna amani na utulivu

68470 Komupic

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu amesema amani, utulivu hautakuwapo nchini Tanzania ikiwa haki itachezewa.

Amesema miaka ya nyuma wananchi waliingia kwenye mapigano dhidi ya wakoloni baada ya kuona utu wao umechezewa.

Komu Ametoa kauli hiyo leo asubuhi Jumamosi Julai 27, 2019 katika mkutano mkuu wa NCCR-Mageuzi unaofanyika jijini Dar es Salaam.

 “Utu inawezekana ndiyo ikawa msingi wa kila kitu hapa duniani, uwepo wetu na kila kitu tunachokifanya ni kwa sababu ya utu wetu.”

“Ili huo utu uende vizuri unahitaji mageuzi katika elimu, uchumi na kila kitu, sasa ili hayo pia yafanikiwe tunahitaji umoja. Ndugu zangu wale wa vyama mbadala mnahitaji zaidi umoja. Tunahitajiana sana,” amesema Komu.

Ameongeza, “Kama Butiku (Joseph- mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere) alivyosema kwa wenzetu mlioko kwenye CCM tunawaomba sana mjifunze na huko duniani mambo yanavyokwenda ili utu wetu tuweze kuushi, Mzee Butiku hakuna amani ,hakuna utulivu hakuna maendeleo katika nchi hii kama hatutaanza kuheshimu utu.”

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz