Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CUF ataka Bunge lichunguze ukweli wa mgawanyo wa mapato

63132 Pic+cuf

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Malindi (CUF) Ally Salehe ametaka Bunge la Tanzania kuunda kamati ya kuchunguza ukweli kuhusu mgawanyo wa mapato kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania Bara.

Akichangia leo Jumatatu Juni 17, 2019 mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Salehe ametaka mapato ya taasisi za muungano yagawanywe sawa.

“Walipokuwa Tume ya Katiba walitaarifiwa kutakuwa na fedha za kuendeshea serikali tatu zingekuwepo. Wanaopinga Serikali tatu wapinge kwa vingine sio kwa uchumi,” amesema.

Amesema makusanyo yanakusanywa Zanzibar ni asilimia 2 na yanayokusanywa Tanzania bara ni asilimia 98 ambayo yote yanatiwa katika kapu moja kwamba zote ni za muungano.

Amesema ACT- Wazalendo walitoa mchanganuo kuwa asilimia 68 ya mapato hayo yanatumiwa na Tanzania bara na kwamba asilimia 32 ndizo zinatumika katika taasisi za muungano.

Amesema kama nchi ilikuwa inaendeshwa sawa basi Zanzibar ilipaswa kupata mgawo wake toka katika asilimia 68.

Pia Soma

“Mwisho na propose (napendekeza) kama hesabu hizi zinabishaniwa basi Bunge liunde kamati ya kuhakikisha ukweli uko wapi?" Amehoji.

Amewataka viongozi kuheshimu Katiba na kwamba hata Serikali ilivyoondoa Ongezeko la Kodi ya Thamani (VAT) kwa umeme unaokwenda Zanzibar haukutarajiwa kusherekewa kwa sababu hakukuwa na uhalali.

“Ili uchumi uende sambamba Zanzibar ipate haki yake, kama si hivyo uchumi wa Zanzibar unadidimia, Serikali ya muungano haiwekezi Zanzibar lakini fedha zote za muungano zinatumika kujenga  Tanzania bara,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz