Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CUF alia kutengwa

36762 Pic+mbunge Mbunge CUF alia kutengwa

Wed, 16 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pemba.Mbunge wa CUF jimbo la Chakechake, Yussuf Kaiza Mamake ameeleza kusikitishwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho katika jimbo lake kushindwa kushirikiana nae ipasavyo.

Akizungumza na Mwananchi, mbunge huyo alisema kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa licha ya kuwa mbunge halali kwenye jimbo hilo lakini anakosa ushirikiano wa kiutendaji kutoka kwa viongozi wa CUF wa jimbo lake.

“Kwa mfano hivi karibuni kulikua na ziara ya katibu mkuu wa chama Maalim Seif Sharif Hamad kisiwani Pemba na jimbo langu ni sehemu iliyotembelewa na kiongozi huyo lakini cha kusikitisha sikupatiwa taarifa kabisa na uongozi wa wilaya wala jimbo,” alisema.

Makame alisema hali hiyo inamsononesha kuona viongozi waliopewa dhamana ya jimbo kushindwa kutambua nafasi yake ndani ya chama na kama kiongozo badala yake amekua akishuhudia shughuli mbalimbali za chama kwenye vyombo vya habari.

‘“Sijui wana njama gani dhidi yangu maana mimi ni kiongozi niliyechaguliwa na wananchi sasa wananinyima fursa hata ya kushiriki kwenye ziara ya viongozi wakuu wa chama chetu,” alisema.

Mbunge huyo amewataka viongozi wa chama hicho kuanzia jimbo hadi wilaya kufuata taratibu za chama chao ikiwamo kuwapatia taarifa viongozi wa majimbo na si kufanya mambo kienyeji kwa lengo la kutengeneza fitina na chuki dhidi ya viongozi kwa wananchi.

Katibu wa CUF wilaya ya Chakechake, Saleh Nassor Juma alisema madai ya mbunge huyo hayana msingi kwani mara kadhaa amemfikishia taarifa za wito mbunge huyo lakini ameshindwa kuhudhuria katika vikao halali vya wilaya na jimbo.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa habari wa CUF, Salim Abdallah Bimani alisema anashangazwa na madai ya mbunge huyo na kwamba chama hakijatofautiana naye.



Chanzo: mwananchi.co.tz