Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CUF alalamikia wananchi kuzuiwa kuandikishwa daftari la Mzanzibar mkaazi

20285 Pic+mbunge TanzaniaWeb

Tue, 2 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Saleh amelaani vikali kitendo cha baadhi ya wananchi wa jimbo lake kuzuiwa kuandikishwa katika uboreshwaji wa vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi visiwani humo.

Saleh ameyasema hayo visiwani Zanzibar leo Oktoba 1, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari akisema jimboni kwake pekee zaidi wa wananchi 300 wamenyimwa haki hiyo.

Amesema kuna ukiukwaji mkubwa wa haki ya kiraia kwa wananchi wa jimbo lake kwani sheria imeweka wazi kila mwananchi aliyefikia miaka 18 anatakiwa kuandikishwa.

Saleh amesema kwamba anashangazwa jinsi masheha wanavyotumika kuwakatalia wananchi wanaokwenda kujiandikisha licha ya kuwa wana haki ya kupatiwa vitambulisho hivyo.

Mbunge huyo amedai kuwa Serikali haiwatendei haki wananchi wake ambao wanahitaji fursa mbalimbali hivyo wanapotokea kunyimwa vitambulisho ni sawa na kukiuka sheria.

Pamoja na hilo, amesema anashangazwa na Serikali kuhusisha shughuli hiyo na masuala ya kisiasa jambo ambalo linawanyima wananchi haki zao.

Mbunge huyo ametoa wito kwa waziri mwenye dhamana, Hajji Omar Kheri kuhakikisha suala hilo linamalizika mara moja na wananchi wapewe haki yao.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz