Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM ataka vionjo mipira ya kiume vitumike kupunguza watoto wa mitaani

64175 Nlinga+pic

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga ametaja sababu za kwa nini kuna ongezeko la watoto wa mitaa akisema chanzo ni watu kutotumia mipira ya kiume na kike wakati wa tendo la ndoa licha ya mipira hiyo kuwekewa vionjo.

Mlinga ameuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumanne Juni 25,2019 kufuatia swali la msingi la Mgeni Jadi Kadika (Viti Maalum- CCM) ambaye aliuliza Serikali ina mkakati gani wa kuokoa kizazi cha watoto wenye mazingira magumu ambao wanakosa haki za msingi ikiwemo elimu.

Akijibu mwaswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile amesema ongezeko la watoto wa mitaani halitokani na watu kutokutumia mipira ya kiume na kike bali linatokana na watu kuzaa katika umri mdogo, uzazi wa haraka kati ya mtoto na mtoto na hali za uchumi.

Amesema hadi Oktoba 2018, watoto wa mitaani walifikia 6,393 wakiwemo wa kiume 4865 na wa kike 1528 wanaotoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Arusha na Iringa.

Naibu Waziri ameziagiza mamlaka za serikali za mitaa ziandae mipango na mikakati madhubuti ikiwemo kutenga rasilimali za kutosha katika kubaliana na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Chanzo: mwananchi.co.tz