Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM amtaka Waziri Kamwelwe ajirekebishe kwa kauli zake

Sat, 10 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaack Kamwelwe ameendelea kuandamwa na wabunge kuhusu majibu anayotoa kwa wabunge wanapomuuliza kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi ya wabunge waliolalamikia majibu ya Kamwele ni Ramadhan Dau (Mafia-CCM), Seleman Bungara (Kilwa Kusini-CUF) na leo Ijumaa Novemba 9, 2018 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka wa fedha 2019/20  Mbunge wa Rufiji (CCM) Mohamed Mchengerwa naye amemtaka kujirekebisha na kurejea katika kasi aliyokuwa nayo wakati akiwa Waziri wa Maji.

“Sisi ni miongoni mwa watu ambao tulimpongeza sana wakati akiwa Waziri wa Maji lakini amekuwa akitoa kauli wakati fulani ambazo haziridhishi,” amesema na kuongeza:

“Nichukue nafasi hii kumweleza ile kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa Waziri wa Maji basi aiendeleze yapo maeneo ambayo mheshimiwa Rais aliweka ahadi ambazo ni sheria zinazohitaji kutekelezwa lakini wewe mheshimiwa waziri ukinijibu kuwa ulioachiwa na Profesa (Makame) Mbarawa huhusiani nayo napata tabu sana.”

Amesema majibu hayo yanamfanya apate tabu sana kumwelewa anawasaidiaje wananchi na kwamba sheria ya uongozi inawataka viongozi kugusa mioyo ya watu wao na wenyewe.

“Nimuombe mheshimiwa waziri arekebishe na arejee katika kasi yake nzuri aliyokuwa nayo wakati akiwa waziri wa maji,” amesema.

Habari zaidi kutoka Bungeni: Msukuma awakosoa maprofesa walioandaa mdahalo wa uchumi

 

Tanzania inadaiwa zaidi ya Sh400 bilioni mahakama za kimataifa

 

 

Mbowe ahoji bungeni ujenzi Daraja la Wami, Serikali yamjibu

 

Chanzo: mwananchi.co.tz