Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM amshukia Waziri Lugola, awatetea polisi Kigoma

26694 Pic+mbunge+ccm TanzaniaWeb

Tue, 13 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima amesema kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuwachukulia hatua viongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma ni ya uonevu.

Amesema hayo bungeni leo Jumatatu Novemba 12, 2018 wakati akichangia mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2019/20  ambao mjadala unamalizika leo.

Mwilima ameanza kwa kutoa pole kwa wananchi wa vijiji vya Mpeta na Mwandubatu kwa maafa makubwa yaliyowakuta yaliyosababisha baadhi ya watu na maaskari kuchinjwa na kufariki dunia.

“Nina imani na Serikali kwa kuwa nimeshalileta mbele ya Spika, Serikali haitakuwa na kigugumizi katika kufanya uamuzi na kutenda haki kwa niaba ya wananchi wangu wa Kigoma Kusini hususani wa kijiji cha Mpeta,” amesema.

Amesema ameanza na suala hilo kwa sababu atazungumzia kuhusu suala la barabara inayopita katika kijiji hicho na kwamba wananchi wake watakapomsikia amezungumzia barabara bila kuzungumzia mateso na manyanyaso  atakuwa hajatenda haki.

Amesema Lugola amefanya uamuzi mzito wa kuwavua vyeo viongozi wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

“Swali langu mawaziri wote waliokwenda wananchi wanasema wakina nani wamehusika katika matukio yale, leo unapowatoa mapolisi wanaopewa amri na mheshimiwa mwenyekiti ni uonevu,” amesema.

“Lazima Serikali ichukue hatua tunataka kama sisi wananchi wa Kigoma Serikali inachukua hatua kwa wahusika wote, wako wanaosema wana viongozi pale Ikulu wanaowatetea, tunataka tuone katika Serikali ya John Pombe Magufuli nani yuko juu yake.”

Amesema wanataka kuona nani anachukua rushwa kwa wafugaji lakini hadi leo hatua hazichukuliwi.

“Mheshimiwa mwenyekiti naiamini Serikali yangu ya CCM, namwamini Waziri Mkuu, namwamini Spika lakini tunataka haki itendeke.



Chanzo: mwananchi.co.tz