Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM alia ujenzi wa mabwawa kujinusuru na njaa

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), Daniel Mtuka amesema hali ya chakula katika Wilaya ya Manyoni ni ngumu na kuiomba Serikali ya Tanzania kujenga mabwawa ili kuepuka njaa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 19,  2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020.

Amesema licha ya Mkoa wa Dodoma kuwa katika eneo lenye ukame, hali ni mbaya jimboni kwake kwa maelezo kuwa upatikanaji wa chakula ni mgumu.

“Pendekezo la mkakati kuondokana na hali ya njaa. Kuna bwawa la tope la Bahi,  lina mito miwili mikubwa inatoka Manyara na lina rutuba ya kutosha,” amesema.

Ameiomba Serikali kuwahisha kukomesha njaa katika eneo hilo kwa kuweka mabwawa ya umwagiliaji

Amesema maji ya kutosha yapo na kwamba kinachotakiwa ni kupeleka watalaam kwa ajili ya kuwachimbia mabwawa.

Pia Soma

Mtuka amesema wanazo ekari zaidi ya 50,000 zenye rutuba zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na kwamba kwa kusaidiwa mabwawa wataweza kulisha na sehemu nyingine.

Mbunge huyo amesema kuna bwawa la kimkakati ambalo tayari andiko lake lipo wizarani na upembuzi ulishafanyika mwaka jana kilichokuwa kikisubiriwa ni ujenzi.

“Ilikuwa iingizwe mwaka jana mkasema itaingizwa (kwenye bajeti) mwaka huu lakini nimeangalia na mwaka huu hakuna,” amesema.

Amesema hataona aibu ya kulia njaa na itakapotokea atafanya hivyo.

Mtuka pia ameomba Serikali kuangalia upya bei ya mbegu za alizeti zao linalotegemewa  linategemewa na wakulima wa Singida.

Amesema bei ya mbegu ni Sh35,000 kwa kilo na wakulima wa Manyoni ni wachovu hawataweza kununua mbegu hizo.

Ameomba Serikali kupeleka ruzuku ili wakulima waweze kunufaika na mbegu hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz