Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM alia na makazi ya polisi

Mbunge CCM alia na makazi ya polisi

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mbunge wa Serengeti (CCM), Marwa Ryoba amemuomba Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuyakumbuka makazi ya polisi wilayani Serengeti kwa kuwa hayapo katika hali nzuri.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 27, 2019 katika ufunguzi wa ofisi ya dawati la jinsia uliofanywa na Sirro.

Amesema nyumba hizo zinatakiwa kufanyiwa ukarabati ili askari polisi waishi katika mazingira mazuri.

“IGP nyumba ya mkuu wa kituo ina nyufa kwa kweli haifai inahitaji ukarabati, pia makazi ya askari si mazuri naomba uwakumbuke," amesema Ryoba.

Chanzo: mwananchi.co.tz