Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM akerwa na matumizi ya ovyo serikalini

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kasulu Mjini (CCM), Daniel Nsanzugwanko amesema bado Serikali ina matumizi makubwa ya ovyo na kumtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuangalia eneo hilo.

Nsanzugwanko amesema hayo leo Jumatatu Juni 3, 2019, wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2019/2020.

Mbunge huyo amesema yeye bado anaamini Serikali ina matumizi makubwa na ya ovyo

“Wakati mwingine masikini watendaji wetu wanatumia magari ya kifahari. Unakuta gari shangingi V8 DFP liko Kasulu kule,  mambo ya ajabu kabisa,” amesema.

Amesema awali mwenendo wa Serikali ilikuwa kupunguza ili kama anavyotaka Rais John Magufuli fedha nyingi ziweze  kupeleka kwenye miradi ya maendeleo.

“Lakini mheshimiwa waziri (Dk Mpango) bado matumizi ya ovyo ya magari ya anasa ambayo hayafai kuwepo katika nchi,” amesema.

Pia Soma

Ametoa mfano wa nchi ya Uganda ambayo hawana mwenendo wa kutumia magari ya anasa.

“Hiyo luxury wameshaiacha. Hatusemi watembee na baiskeni no (hapana),  hiyo ni kupotosha. Hivi kwa mfano unampaje Region Manager wa Tanroad (Meneja wa Mkoa wa Wakala wa Barabara) V8 shangingi why (kwa nini)?,”amehoji.

“Kwanini usimpe a good pick up car (gari zuri la Pick up) akikuta bango limeanguka anabeba bango lake? Kwanini umpe V8 nani anaiservice gari ile? Hoja ya msingi nenda ukaangalie bado matumizi ya ovyo ni makubwa sana.”

Chanzo: mwananchi.co.tz