Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM akataa majibu ya Serikali ya Tanzania

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Serengeti (CCM) Marwa Chacha leo Jumatano Juni 26,2019 ameyakataa majibu ya Serikali ya Tanzania kuhusu ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara.

Katika swali la msingi Marwa ameuliza Serikali ina mpango gani dhidi ya ukamilishaji wa barabara hiyo na lini wananchi waliofanyiwa tathimini watalipwa fidia zao.

Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amekiri barabara hiyo kuchelewa kukamilika tangu ilipoanza kujengwa mwaka 2013.

Naibu Waziri amesema zipo sababu mbalimbali zilizopelekea barabara hiyo kutokamilika kwa wakati ambapo serikali imeshachukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika mapema.

Kuhusu fidia kwa wananchi amesema watu 8 wameshalipwa Sh 12.87 Milioni wakati wengine 433 wamelipwa fidia ya Sh2.6 bilioni katika eneo la Makutano- Sanzate yenye kilomita 50.

Chanzo: mwananchi.co.tz