Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM aitaka Serikali kuongeza ruzuku kwa halmashauri

40353 Mbungepic Mbunge CCM aitaka Serikali kuongeza ruzuku kwa halmashauri

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Mpwapwa (CCM) George Lubeleje amehoji iwapo Serikali iko tayari kuongeza ruzuku katika halmashauri ili waweze kuongeza posho za madiwani.

Lubeleje amehoji hayo leo Jumanne Februari 6, 2019, ambapo amesema Serikali kuu imechukua vyanzo vyote vya mapato.

“Serikali imechukua vyanzo vya mapato, makusanyo yatatoka wapi? Kwa nini Serikali isiongeze ruzuku kwa halmashauri ili waweze kuongeza posho,” amesema.

Lubeleje pia amehoji kwa nini Serikali isiwaweke madiwani katika sheria ya mafao ya wanasiasa.

“Wakati wa uchaguzi tunakuwa mafiga matatu lakini ukishaisha wanakuwa watu wa kawaida,” amesema.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara amesema kwa kuwa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2019/20 yanaendelea, halmashauri ziangalie jinsi ya kuongeza mapato.

Kuhusu kuwaingiza katika sheria ya mafao ya wanasiasa, Waitara amesema ni utaratibu lakini wako tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.

Waitara amesema mwaka 2013/2014 Serikali ilipandisha posho za madiwani kutoka Sh250,000 hadi Sh350,000 na wenyeviti kutoka Sh 350,000 hadi Sh400,000.

“Ongezeko la posho na maslahi ya madiwani litatokana na halmashauri kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani,” amesema.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz