Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM ahojiwa Takukuru Moro

Moromp.webp Mbunge CCM ahojiwa Takukuru Moro

Wed, 10 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Morogoro inamchunguza Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Christine Ishengoma, kutokana na tuhuma za kutoa rushwa kwa wapiga kura, huku ikiwahoji watu mbalimbali kutokana na tuhuma hizo.

Aidha, Takukuru imewafikisha Mahakamani aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Boma, Amir Nondo, na wenzake watatu kutokana na makosa ya uhujumu uchumi baada ya kudaiwa kubadili matumizi ya kiwanja eneo la msamvu bila kufuata taratibu za mipango miji.

Nondo anadaiwa kufanya kosa hilo wakati akiwa kwenye nafasi ya uenyekiti wa kamati ya mipango miji na mazingira.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Janet Machulya, ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na amewaonya wananchi wanaotaka nafasi za uongozi kuacha kupita pita na kutoa rushwa.

Pia amewataka watumishi wanaoaminiwa wakiwemo wenye dhamana ya usimamizi wa ardhi kuacha kufanya udanganyifu katika michakato ya kumilikisha ardhi na kusababisha migogoro kutokana na udanganyifu kitu ambacho kitwafanya kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live