Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM ahoji uhalali mahabusu kusafirishwa kwa bodaboda

93415 Mlinga+pic Mbunge CCM ahoji uhalali mahabusu kusafirishwa kwa bodaboda

Wed, 29 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Ulanga (CCM) nchini Tanzania, Goodluck Mlinga amesema kutokana na ukosefu wa usafiri katika Gereza la Ulanga mkoani Morogoro, askari wamekuwa wakitumia bodaboda kuwasafirisha mahabusu kwenda mahakamani.

“Nilini Serikali itapeleka gari katika gereza la Ulanga,” amehoji Mlinga.

Kabla ya kumruhusu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad  Masauni kujibu, Spika wa Bunge, Job Ndugai akasema, “hii ni mpya kama mambo haya yapo.”

Akijibu, Masauni amesema watatatua changamoto ya ukosefu wa magari kadri yatakapopatika na kwamba yakipatikana watapeleka katika gereza la Ulanga.

Naye Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) Esther Matiko amehoji ni lini Serikali itapeleka nguo kwa ajili ya wafungwa.

Amesema katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam kutokana na kukosekana kwa nguo, jambo ambalo limesababisha askari wa magereza kuwapa nguo zao wanapotoka nje.

Pia Soma

Advertisement
Akijibu swali hilo, Masauni amesema wafungwa wamekuwa wakipewa sare na kwamba changamoto hiyo itakuwa ikipungua hatua kwa hatua.

Chanzo: mwananchi.co.tz