Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM ahoji katikakatika umeme Dar

60321 Pic+umeme

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Temeke (CCM), Abdallah Mtolea ameitaka Serikali kueleza ni mkakati iliyonayo  kumaliza tatizo sugu la kukatika umeme mara kwa mara katika jiji la Dar es salaam.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya nishati kwa mwaka 2019/20 ya Sh2.14 trilioni bungeni jana, mbunge huyo alisema licha ya mawaziri wa wizara hiyo, Dk Medard Kalemani na naibu wake, Subra Mgalu kufanya kazi kubwa, lakini bado kuna tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme Dar es Salaam.

“Kukatikakatika kwa umeme katika Jiji la Dar  es Salaam imekuwa ni kero kubwa, ni ngumu sana kukaa siku nne bila umeme kukatika,” alisema Mtolea.

 

Alisema aliwahi kuhoji tatizo hilo linachangiwa na nanini, akajibiwa kituo cha kupozea umeme cha Mbagala na Kigamboni kuna tatizo.

 

Pia Soma

“Sasa maana yake bado hatujapata dawa ya kutatua tatizo hili, Dare es Salaam ndio soko kubwa sana kwani MW 600 za umeme ziko Dar es Salaam na watumiaji wakubwa wapo Dar es Salaam.”

 

“Serikali ije na mpango mzuri wa kuhakikisha wanalitibu tatizo hili na ukipiga simu (Tanesco) unaambiwa transfoma imezidiwa, nguzo zimeanguka, sasa ni ama hatujui wateja tulio nao au kuna nini.”

 ‘Wateja wa Dar es Salaam wanaingizia fedha nyingi Tanesco ikiwa umeme utapatikana kwa wakati. Umeme ukikatika hata nusu saa tu kwa Dar es Salaam Tanesco inapoteza mapato hivyo ningependa kupata mkakati madhubuti wa dawa ya umeme kukatikakatika,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz