Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Bwege ataja mambo yatakayoipatia ushindi CCM uchaguzi mkuu 2020

94726 Bwege+pic Mbunge Bwege ataja mambo yatakayoipatia ushindi CCM uchaguzi mkuu 2020

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara maarufu Bwege ametaja mambo kadhaa aliyodai kuwa kama yakifanyika yatakipa ushindi CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Februari 6, 2020 mbunge huyo amesema katika sekta ya umeme, Serikali ya Tanzania imefanya vyema huku akitaja baadhi ya mambo anayodai kuwa hayafanyiki kama inavyotakiwa.

Mbunge huyo ambaye kila anapozungumza bungeni huwa kivutio kutokana na staili yake ya kutamka maneno kwa ukali, upole, kufoka, kucheka na kununa kwa pamoja, aliwafanya wabunge kuangua kicheko huku Spika Job Ndugai akihoji kwa masihara kuwa muda wake wa kuchangia umekwisha.

“Kwa umeme..., kwa umeme mmetufikisha mahali pazuri, na kama mtaendelea hivi kuhusu umeme na mtafanya spidi katika maji, mkawalipa makandarasi wa umeme vizuri,  mkawalipa wakulima wa korosho fedha zao zote. Mkaongeza  mishahara kwa wafanyakazi, kesi za kubambikia hakuna, ikawa maandamano yapo ipo..., aaah CCM mnashinda.”

“Na masheikh waliokuwa ndani miaka minane mkawaachia aaah CCM dole. Lakini kama sifa yenye umeme lakini  masheikh hawatoki, mishahara hamuongezi, wakulima hamwalipi hesabuni kuumia tu 2020.”

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz