Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Bwege adai wanyonge hawataichagua CCM 2020

64026 Pic+bwege

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara maarufu Bwege amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 Watanzania wanyonge hawataichagua CCM kwa madai Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli haiwatendewi haki.

Bungara ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 24, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Serikali ya Tanzania mwaka 2019/2020 ya Sh33.1 trilioni.

Mbunge huyo amedai wanyonge ni wafanyakazi, wakulima, wavuvi na wafanyabiashara, kwamba makundi hayo yanalia kutokana na kubanwa katika maeneo mbalimbali na kushindwa kufikia malengo yao.

“Kwanza wavuvi kule Kilwa wanatozwa ushuru wa Sh3,300 katika kila kilo moja ya dagaa wakati kule ziwa Victoria wavuvi wanatozwa Sh300. Jambo hili linawafanya wavuvi wa Kilwa kushindwa kufikia malengo yao,” amesema Bwege.

Amesema hoja kuwa wafanyakazi kutoongezewa mshahara ili Serikali itekeleze miradi mikubwa si sahihi huku akitolea mfano posho na mshahara mkubwa wanaolipwa wabunge.

“Mbunge hata asipoongezewa mshahara atakula vizuri, atakunywa maji safi lakini si hawa wananchi. Tazama katika kilimo mmetenga kiasi kidogo cha fedha za maendeleo wakati mkijua kuwa Watanzania wengi ni wakulima.”

Pia Soma

“Watu wanapigwa risasi eti Serikali ya wanyonge, mkulima wa korosho hajalipwa eti Serikali ya wanyonge. Hivi mnapitaje katika uchaguzi ujao. Wakulima, wavuvi, wafanyakazi na wafanyabiashara wote wanalia. Wanyonge hawawezi kuichagua CCM mwaka 2020, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,” amesema Bwege.

Chanzo: mwananchi.co.tz