Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge: Bajeti ya kisayansi inayopanua wigo wa kodi

Mbunge Mbunge: Bajeti ya kisayansi inayopanua wigo wa kodi

Mon, 21 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akichanga bajeti hiyo mwishoni mwa wiki bungeni jijini Dodoma, mbunge huyo alihamasisha Watanzania kuipokea ili ikalete mabadiliko ya nchi yao.

"Dunia nzima hakuna nchi isiyolipa kodi ila inategemea ni kodi za aina gani ambazo wananchi watazimudu, mfano kodi ya majengo nimesikia kuna watu wanaiongelea wakisema italeta mkanganyiko baina ya mwenye nyumba na mpangaji,” alisema na kuongeza;

“Nchi hii ina wataalamu na nyumba zetu zina hati kwa hiyo wataangalia nyumba hii hati ni ya nani, niwatoe wasiwasi Watanzania wanaosema huu ni mkanganyiko."

Munde alisema ikitokea kwa bahati mbaya mpangaji akakatwa kodi ya jengo stakabadhi itaandikwa ili siku atakapoanza mkataba mpya na mwenye nyumba wataiweka mezani ili ikatwe kwenye mkataba.

Aliwataka Watanzania kuzipokea kodi hizo kwa sababu hazilengi kuwaumiza badala yake serikali itaongeza mapato na kutekeleza shughuli za maendeleo.

"Tunahitaji Sh. trilioni 36 ili kutekeleza shughuli za maendeleo ni lazima Watanzania tulipe kodi hatuwezi kuwa na nchi ambayo wananchi wake hawalipi kodi tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu suala la kodi ya simu siyo kweli mtu akiamka asubuhi anakatwa bali akiweka muda wa maongezi watakatwa kuanzia Sh. 10 na kuendelea," alisema.

Alisema ukusanyaji wa kodi wa aina hiyo utaiwezesha Tanzania kupiga hatua kimaendeleo.

Kuhusu bodaboda Munde alisema kundi hilo kwa muda mrefu lilikuwa linaumia na kodi kubwa ya Sh. 30,000 na kwamba serikali imewapunguzia mzigo mkubwa.

"Suala la madiwani kulipwa posho moja kwa moja na serikali ni jambo zuri kwa sababu watapata fedha zao kwa wakati muafaka kwa sababu madiwani wangu wana miezi sita hawajalipwa," alisema.

Kadhalika, alisema tangu uhuru haijawahi kutokea awamu ikalipa posho ya madaraka kwa Mtendaji Kata na Katibu Tarafa na kuomba suala hilo liungwe mkono.

Chanzo: ippmedia.com