Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Ataka Wafungwa Waende na Magodoro Gerezani

Mbunge 1.png?fit=700%2C400&ssl=1 Mbunge Ataka Wafungwa Waende na Magodoro Gerezani

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Songwe Neema Gerald, amesema kuwa ili kuipunguzia serikali mzigo wa kununua magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu gerezani, basi ione haja ya wafungwa hao kuwa wanaenda na magodoro yao.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo hii leo Septemba Mosi, 2021, Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Tunafahamu kabisa Magereza kuna changamoto ya magodoro na serikali inawajibika kuhakikisha magodoro yanakuwepo, sasa haioni haja ya mahabusu au wafungwa wote wakawa na kigezo cha kwenda na magodoro yao ili waweze kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro Gerezani, kwa sababu siyo wote wanashindwa kuwa na magodoro kuliko kuiongezea serikali mzigo,” amesema Mbunge Neema.

Chanzo: globalpublishers.co.tz