Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ACT Wazalendo amsifu JPM, aponda wanaotaka aongezewe muda (+video)

Screenshot 2021 02 09 At 16.02.10 660x400.png Mbunge ACT Wazalendo amsifu JPM, aponda wanaotaka aongezewe muda (+video)

Tue, 9 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, amemwagiza Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole, aende akawaambie wana CCM ambao bado wanataka Rais Dkt. Magufuli, aongeze muda wa madarakani kwamba alikwishasema hawezi kuongeza muda hivyo wasimlazimishe.

Mbunge wa Konde kupitia Chama cha ACT Wazalendo Khatib Haji, amemwagiza Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole, aende akawaambie wana CCM ambao bado wanataka Rais Dkt. Magufuli, aongeze muda wa madarakani kwamba alikwishasema hawezi kuongeza muda hivyo wasimlazimishe. “Magufuli atakuwa ni Rais wa kwanza kwa nchi za Afrika ambaye baadhi ya wabunge wake wanamuomba aongeze muda lakini tayari ameweka msimamo. Polepole waambie CCM Rais hana shida ya kuongeza muda alikutuma na video zinatembea tunaziona kwanini unawaacha akina Sanga hapa wanaendelea kupotosha?, kwanini hamuheshimu mawazo ya Mh. Rais?”,  Mbunge Khatibu.Akijibu hoja hiyo Polepole amesema kuwa, “Mimi naomba nitumie nafasi hii kumpa taarifa Mbunge, kwamba masuala ya CCM yanzungumziwa kwenye vikao vya chama hapa Bungeni, wabunge wana uhuru wa kutumia uhuru wa Bunge kuzungumza lakini kinachozungumzwa hapa ndani hakiathiri msimamo wa chama tumekwishautoa Rais hataongeza muda”.

Chanzo: millardayo.com