Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe mwenyekiti mpya wa CCM Ubungo

Owe Pic Data Mbowe Mwenyekiti mpya wa CCM Ubungo

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya mgombea mwenzake wa nafasi hiyo Rogati Mbowe kushinda kwa kura 407.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba 3, 2022, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Galik Ramadhani alisema kura zilizopigwa ni 732 kati ya hizo mbili ziliharibika.

"Rogati Mbowe amepata kura 407, Lucas Mgonja amepata kura 288, William Masanja kura 27 na Theresia Chihota kura nane hivyo napenda kumtangaza Rogati Mbowe kuwa mshindi wa nafasi hiyo,"

Baada ya uchaguzi huo kuisha na matokeo mwenyekiti huyo mpya wa wilaya ya Ubungo aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kuwataka kuvunja makundi na kuungana pamoja kukijenga chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live