Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe kuzindua Kanda ya Nyasa, mikutano ya hadhara

Chadema Hadhara Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa William Mungai akizungumza kuhusu uzinduzi

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe anatarajiwa kuzindua rasmi kanda ya Nyasa Februari 23 wilayani Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na kisha kufungua mkutano wa hadhara mkoani Iringa Februari 28 mwaka huu.

Hayo yameelezwa Jumanne Februari 21, 2023 na Mwenyekiti wa Chadema wa mkoa huo, William Mungai wakati akizungumza na Mwananchi digital, akisema kabla ya mkutano huo ni sehemu ya mikutano ya hadhara itakayofanywa katika miji, kata na vijiji.

"Mkoa wa Iringa ni Moja kati ya Mikoa mitano ambayo ipo katika kanda ya Nyasa ambapo uzinduzi mkubwa utafanyika Februari 23 mwaka huu wilayani Sumbawanga na Kamati kuu ya chadema itakuwepo," amesema Mungai.

Amewaomba wanachama wa chama hicho na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mkutano huo, akisema ndiyo njia ya kuitumia demokrasia.

"Mkoa wetu tumejiandaa ipasavyo kufanya mikutano ya hadhara ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi February 28 mwaka huu, hivyo tunaendelea na màandalizi kwa sababu tutaanzi kutubia Mafinga kisha Iringa Mjini kwa ajili ya uzinduzi wa Mkutano hiyo," amesema Mungai.

Mwenyekiti huyo Amefafanua kuwa baada ya uzinduzi huo, Mikutano hiyo itahamia kwenye Wilaya na majimbo yote hadi ngazi ya kata pamoja na vijiji.

Kwa upande wake mkazi wa Mafinga, Fredy Mgaya ameishukuru Serikali kwa kufungua mikutano ya kisiasa kwani inawasaidia kujua mwelekeo wa nchi na haki zao.

"Tunaishuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa vyama vya siasa na kufungua Mikutano kwa sababu inatusaidia sisi kama wananchi kujuwa mambo mbalimbali ya Serikali kupitia mikutano hiyo,

Chanzo: Mwananchi