Hai. Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe kuanzia leo Ijumaa Februari 28, 2020 atafanya mkutano wa hadhara katika jimbo hilo kwa siku tano mfululizo.
Akizungumza na Mwananchi jana Alhamisi Februari 27, 2020 katibu wa Chadema Wilaya ya Hai, John Munis amesema polisi wamewapa kibali cha kufanya mikutano hiyo.
“Mbowe atakuwa na mkutano wa hadhara, atazungumza na wananchi wake pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili.”
“Mikutano hiyo itafanya kwa siku tano mfululizo, kuanzia kesho Ijumaa hadi Jumanne ijayo katika sehemu mbalimbali za Wilaya ya Hai,” amesema Munis.
Amesema kesho Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atafanya mkutano katika viwanja vya Nkoromu kata ya Masama kati.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema polisi wana taarifa ya mkutano huo.
Pia Soma
- Askari aliyembaka mtoto wa askari mwenzake afukuzwa kazi
- Tanzania yashinda kwa hifadhi bora duniani
- UBUNIFU: Msichana anayetumia teknolojia kubuni programu