Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe bado hajakubaliana kukamatwa kwake

Mbowe Ed.jpeg Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Wakati kesi ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ikitajwa mahakamani leo, kiongozi huyo amekuja kivingine akifungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu dhidi ya Serikali akipinga taratibu za kukamatwa na kushtakiwa kwake.

Miongoni mwa madai yake, Mbowe anapinga kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi kimyakimya bila kumtaarifu kwanza kuhusu mashtaka hayo pamoja na maneno ya vitisho anayodai kupewa na polisi kabla ya mashtaka hayo.

Vilevile mwanasiasa huyo anelalamikiwa haki zake kukiukwa kwa ndugu na wakili wake kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilishwa.

Mbowe anadai wakati ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa ofisa wa polisi.

Kabla ya hatua hiyo Mbowe alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano tangu alipotiwa mbaroni Julai 21, 2021 usiku akiwa jijini Mwanza alikokwenda kwa maandalizi ya kongamano la kudai Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Baraza a Vijana wa Chadema (Bavicha).

Usiku huohuo alisafirishwa mpaka Dar es Salaam hadi nyumbani kwake ambako alifanyiwa upekuzi kisha akashikiliwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay hadi alipopandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi kimyakimya katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka 2020..

Chanzo: Mwananchi