Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe awataka wananchi kujiandaa na uchaguzi

Mbowe 255 255 Mbowe awataka wananchi kujiandaa na uchaguzi

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka wananchi mkoani Mwanza kujipanga na kuwaunga mkono kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2024/25.

Mbowe alitoa kauli hiyo alipokuwa Malya wilayani Misungwi juzi Jumatano, katika mwendelezo wa mikutano ya ‘+255 Katiba Mpya, Okoa Bandari Zetu’ huku akiwataka wananchi kujipanga na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Mungu ameshatuletea neema katika uchaguzi ujao kabla ya misa ya kwanza kuisha, tushamaliza shughuli, nikiangalia sura hizi naona viongozi wazuri wa kesho, madiwani, wabunge, wenyeviti wa vijiji na vitongoji,” alisema Mbowe.

Pia, alisema chama hicho sio chake, ni cha wananchi, hivyo wajipange na kutumia chama hicho ili kiwaletee viongozi wenye hofu ya Mungu na watakaoweza kubadilisha maisha ya wananchi.

“Tumieni chama hiki, kwanza kinasimamia misingi minne ya kwanza, hiki ni chama kinachosimamia haki za wakulima, wafugaji, haki za wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na haki za kila mmoja,” alisema Mbowe.

“Ni chama kinachopigania uhuru na demokrasia katika nchi yetu na ni chama kinacholinda amani na furaha kwa kila mmoja, piganieni chama hiki mkaunganishe nguvu ya kila mmoja, Mungu amewapa Kanda ya Ziwa na kila rasilimali mnazohitaji.” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live