Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe awataka CCM kutubu dhambi, kujiunga CHADEMA

Mbowe Mkutanoni Mwanza Mbowe awataka CCM kutubu dhambi, kujiunga CHADEMA

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amewakaribisha wanachama na viongozi wa vyama vingine vya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiunga na Chadema ili kukiondoa chama tawala madarakani.

Mbowe ametoa ukaribisho huo leo alipokuwa akihutubia wananchi wa Kata ya Kakonko mjini mkoani Kigoma, ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni +255 Katiba Mpya iliyozinduliwa Mei 17, 2023 Kitaifa mkoani humo.

"Kama kuna masalia ya vyama vingine vidogo vidogo ambavyo vimeshakosa mwelekeo karibuni kwenye jeshi la ukombozi, Jeshi la Chadema; tuunganishe nguvu hata wale wa Chama Cha Mapunduzi wanaopenda haki na wanaoamini kwamba haki hunyanyua Taifa karibuni Chadema tubuni dhambi zenu tusonge mbele kukomboa taifa letu," amesema.

Mwanasiasa huyo ambaye ni mmoja wa waasisi wa chama hicho cha upinzania, amewataka wana Chadema ambao ni waathiriwa wa vitendo vya uminyaji wa Demokrasia nchini, kusahau maumivu waliyopitia na kuanza safari ya mapambano upya ili kuikomboa nchi kutoka kwenye mikono ya CCM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live