Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe awasili kwenye mkutano

97462 Mbowe+pic Mbowe awasili kwenye mkutano

Sat, 29 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe amewasili katika viwanja vya Nkoromu kata ya Masama Kati kwenye mkutano wa hadhara na kupokelewa na mamia ya wananchi.

Leo Ijumaa Februari 28, 2020 Mbowe ameanza ziara ya ya siku tano katika jimbo hilo kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Hai, John Munis amesema polisi wamewapa kibali cha kufanya mikutano hiyo.

“Mbowe atazungumza na wananchi wake pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili. Mikutano hiyo itafanya kwa siku tano mfululizo, kuanzia leo Ijumaa  hadi Jumanne ijayo katika sehemu mbalimbali za Wilaya ya Hai,” amesema Munis.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema polisi wana taarifa ya mkutano huo.

'”Kiutaratibu mbunge  anapokuwa na mikutano yake  anapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi wilaya na taarifa za mkutano wa Mbowe tunazo,” amesema Kamanda Hamduni.

Pia Soma

Advertisement
 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz