Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe awaomba radhi wanawake kwa kuwaita 'mademu'

Mbowe Musomaa Freeman Mbowe

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewaomba radhi wanawake kwa kuwaita mademu wakati anahutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Jumamosi iliyopita jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Mara leo tarehe 23 Oktoba 2023, Mbowe amesema kauli hiyo imewakwaza baadhi ya watu kwa sababu haikuwa ya staha.

“Kuna jambo napenda niliseme, nilizungumza katika mkutano siku mbili zilizopita nikazungumza katika kujenga hoja yangu nikajenga hoja nikawazungumzia mama zetu kama mademu, kuna watu nimewakwaza kidogo na mimi naelewa haikuwa lugha ya staha lakini kiongozi mstaarabu hawezi kuogopa kuomba radhi, wale wote waliofikiri lugha ile niliitumia vibaya naomba radhi ndugu zangu,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema chama chake kinawapenda na kuwathamini wananwake, hivyo kitaendelea kuimarisha usawa wa kijinsia.

Akizungumzia ajenda za kitaifa, Mbowe amesema nchi inahitaji katiba mpya iliyo bora ambayo itakuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wanaokiuka maadili yao ya kazi.

“Lazima tupate katiba mpya ambayo kiongozi akifanya maamuzi ya kihuni lazima yakamtafune mbele ya maisha, ili kila mmoja anayepewa ofisi ya umma ajue anakabidhiwa roho za watanzania, hayo ndiyo mabadiliko ya msingi tunayotaka katika nchi yetu,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Tunataka viongozi wetu hata wa Chadema wanapokamata madaraka ya umma wawe na hofu ya Mungu wanapoongoza, katiba iwadhibiti viongozi wetu wanaotumia madaraka vibaya kwa kutoa amri za watu kuuawawa na kujeruhiwa, watambue kwamba mbele ya safari watajibu maswali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live