Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe atetema 'Serikali inajikwaa ikiiona CHADEMA'

Mbowe IWD Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe amesema ili kupata amani katika maeneo yote nchini ni muhimu kama taifa kutenda haki ili kuleta usawa katika nyaja zote muhimu kijamii.

Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kitaifa kwa chama hicho mkoani Iringa leo Machi, 08, 2022.

Mbowe ameeleza kuwa moja ya hoja alizowasilisha wakati alipokutana na Rais Samia mapema mara baada ya kutoka gerezani ni suala la Haki ili kuleta usawa kwani kumekuwepo na tabia iliyorithika kwa viongozi wengi wa kiserikali na kidini kuhubiri na kutangaza kuhusu amani pasipo kusema zaidi kuhusu Haki.

Akitoa majibu kuhusu kile kilichotokea mapema mjini hapo kufuatia agizo la RPC mkoa wa Iringa kutoa agizo la kushushwa kwa bendera zote za CHADEMA kisha kuwekwa bendera za CCM pekee, Mbowe amesema kuwa vitendo kama hivyo ndivyo vinavyoua demokrasia na kuwa sio makubaliano waliyofikia katika mazungumzo yake na Rais Samia.

"CHADEMA ikipiga hatua ndipo vikwazo zinazidi kuwa vingi, Serikali inajikwaa ikiiona CHADEMA"

"Njia sahihi na ya kidemokrasia ya kutafuta haki katika Taifa hujengwa kwanza kwa kuwepo nia ya kweli ya kisiasa (political will). Kisha ni mchakato wa majadiliano ya kutengeneza mifumo ya kutekeleza azma hiyo. Huku ndiko mazungumzo yetu yalipojikita."

"Haki ni dhana pana sana. Tulikubaliana kuwa haki hizi haziwezi kupatikana kwa tukio la kikao kimoja. Tulikubaliana kikao kile kiwe cha kuweka msingi imara wa kuanza kujenga kuaminiana na isiwe kwa maneno tu bali kwa matendo."Amsema Mbowe

Mbowe ameongeza kusema kuwa Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kusimama hadharani kutangaza nia ya dhati ya kurejesha haki ya kweli nchini.

"Mama amekuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu baada ya ujio wa pili wa vyama vingi mwaka 1992, kusimama hadharani na kutamka nia njema ya kukiri kutanguliza haki katika kuijenga Tanzania mpya yenye amani endelevu. Nawaomba Watanzania wenzangu wote waridhie msingi huu." Mbowe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live