Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe ataja mambo matatu aliyozungumza na Rais Samia

Mbowepic Siasa Leo Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametaja mambo matatu waliyozungumza na Rais Samia Suluhu Hassan walipokutana Machi 4, 2022 baada ya kutoka gerezani, ikiwamo kujadili njia bora ya kutafuta amani na suluhisho katika kufanya siasa.

Mbowe ameyasema hayo leo Machi 18 jijini Dar es Salaama alipokuwa akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Machi 16 jijini hapa.

Amesema; “Tulikubaliana aache kuzungumzia neno amani azungumze neno haki. Jambo la tatu nilimfahamisha yeye apende au mtu mwingine Chadema ni Chama Kikuu cha Upinzani huwezi kukiacha nje.”

Akisisitiza kuhusu hoja hiyo, amesema chama hicho kipo kila mahali na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vingine haviwezi kuinyamazisha.

“Mambo mengine Nilimwambia tutazungumza baada ya kukutana na chama changu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live