Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe asema Chedema ikishika madaraka, hakutakuwa na ubaguzi wa elimu

Lughapic Data Freeman Mbowe akisalimiana na wananchi wa Hai

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema chama hicho kikishika dola kitabadilisha mfumo wa elimu nchni na kuhakikisha Lugha ya Kiingereza inakuwa lugha ya kufundishia kuanzia madarasa ya awali hadi chuo kikuu.

Mbowe ameyasema hayo Jumamosi Machi 19, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya ofisi za chama hicho zilizopo Bomang'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Amedai elimu inayotolewa kwa sasa haimjengi mtanzania kuingia katika ushindani wa soko la ajira, kutokana na mfumo wa elimu uliopo kwa sasa.

"Kumekuwa na ubaguzi katika elimu, iko hivi, viongozi wetu wamekuwa wakituhubiria tujifunze kiswahili ni lugha yetu ya Taifa, lakini leo kiswahili hicho kinazungumzwa kwenye shule zetu za kata, viongozi wote na watu wenye uwezo wanasomesha watoto katika shule za mfumo wa kiingereza"

"Chadema tukiingia madarakani, kiingereza ni lugha ya kimataifa, lazima watoto wote wafundishwe na kiingereza kiwe sehemu ya masomo kuanzia chekechea kwa kila mtanzania, hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live