Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe apata pigo, akimbiwa na wenyeviti 13

53052 WENYEKITI+PIC

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Wenyeviti wa vitongoji 13 katika Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wanaotokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wenyeviti hao wamechukua uamuzi huo leo Alhamisi Aprili 18,2019 wakidai wameridhishwa na utendaji kazi wa Serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Viongozi hao wanaotoka jimbo linaloongozwa na Freeman Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema wamepokelewa na kukabidhiwa kadi za CCM na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai, Wang'uba Maganda.

Aidha baadhi ya wenyeviti hao, wameeleza kuwa wakati walipoingia kwenye chama hicho (Chadema) walitegemea watawaletea wananchi maendeleo na badala yake waligonga mwamba kutokana na chama hicho kuwa na migogoro mingi isiyoisha.

"Tangu tujiunge Chadema hakuna maendeleo yoyote tuliyowaletea wananchi wetu zaidi ya migogoro, hivyo kutokana na utendaji kazi mzuri wa Rais wetu na serikali yake kwa ujumla tumeona ni vyema tukajiunga na CCM ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kweli," Ryandumi Kimaro, ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Uswaa

Majina ya wenyeviti wa vitongoji waliojiunga CCM ni Gladson Swai (Bomani), Ryandumi Kimaro (Makiweru), Beda Msofe (Lembeni), Ndemael Massawe (Nure), Leonard Urassa (Njoro chini) na Raymond Mushi (Mkwalengia).

Wengine ni; Filbert Usiri (Mkwamandaa), Eliatosha Lema (Masaeni), Majisi Paulo (Ngulu juu), Nimkaza Mhando (Kikuletwa), Gasper Mwasha (Bomani Kati), Wolter Swai (Masam) na Majisi Nyange (Lembeni A).

Awali akiwakabidhi kadi za chama hicho, Maganda amewapongeza viongozi hao kwa kufanya uamuzi wa kishujaa kujiunga na chama hicho.

Kwa upande wake, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basili Lema amesema kuwa ni furaha yao kuona wanaondoka wachache alafu wanarudi wengi ,hivyo wanahitaji kwenda kwenye uchaguzi  na watu ambao wako tayari kufanya kazi ya ukombozi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz