Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe akutana na Balozi wa Marekani, wajadili demokrasia

Mbowe Marekani Balozi.png Mbowe akutana na Balozi wa Marekani, wajadili demokrasia

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Wawili hao wamejadili masuala ya mabadiliko ya kidemokrasia nchini Tanzania, kwa mujibu wa Balozi Battle aliyeandika ujumbe katika ukurasa wake wa X (zamani Twitter).

“Nimefurahi kuungana tena na Freeman Mbowe kujadili maendeleo ya mabadiliko ya kidemokrasia nchini Tanzania,” ameandika Balozi Battle.

Mbowe amekutana na Balozi Battle ikiwa zimepita siku chache tangu alipotangaza kufanyika kwa maandamano nchi nzima Januari 24, 2024 kushinikiza Serikali kuondoa miswada mitatu ya sheria za uchaguzi alizodai haijazingatia maoni ya wananchi.

Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana, Novemba 3, 2023 walikutana ambapo Mbowe katika ukurasa wake wa X aliandika akieleza kwamba miongoni mwa mengi waliyojadili, ni changamoto kadhaa zinazokabili ujenzi wa demokrasia nchini Tanzania.

Pia, amemshauri kuhusu umuhimu wa kuendeleza juhudi shirikishi zitakazowezesha ujenzi wa demokrasia imara itakayoweka misingi ya maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii nchini Tanzania.

Aidha, amemueleza Balozi hofu yake kuhusu uharibifu wa mazingira katika Mlima Kilimanjaro na mfumo wake wa ikolojia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live