Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe akamatwa na polisi, asema anapitia kipindi kigumu

97459 Pic+mbowe+3 Mbowe akamatwa na polisi, asema anapitia kipindi kigumu

Sat, 29 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Polisi Wilaya ya Hai wamemkamata Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika viwanja vya Nkoromu Masama kati wilayani humo.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alikamatwa saa 12:00 baada ya kumaliza mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wananchi.

Wakati akijiandaa kuondoka eneo hilo, polisi walikwenda katika gari lake wakieleza kuwa wanamhitaji kituoni, ombi ambalo liliridhiwa na mwenyekiti huyo wa Chadema.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Mbowe amesema licha ya kupitia  kipindi kigumu na changamoto mbalimbali za kisiasa, hawezi kukoma kuendelea na mapambano.

Huku akisisitiza kuwa hajawahi kupitia kipindi kigumu katika siasa kama sasa, Mbowe amesema, “kufa sijafa lakini cha mtemakuni nimekiona, nimekaa jela, mahabusu na mahakamani nimekwenda lakini sikomi ng'o, ndio kwanza wananitia moto.”

Amesema haogopi haogopi kufa wala kwenda jela, huku akigusia umuhimu wa kujenga miundombinu ya barabara na reli na kuwaacha wananchi kuwa huru.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
"Hakuna kitu chenye thamani katika maisha yenu kama uhuru wenu, mkijengewa barabara, shule lakini mkanyimwa uhuru wenu ni bora mvikose hivyo vyote lakini mpate uhuru wenu na hayo ndiyo maneno ambayo Chadema tumehubiri,” amesema Mbowe.

Mbowe leo ndio ameanza ziara ya siku tano katika jimbo la Hai inayoambatana na mikutano ya hadhara, na amebainisha kuwa kesho Februari 29, 2020 atazungumza mapema na wananchi wa eneo la Bomang'ombe.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz