Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe ajilipua baada ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya siasa

Mbowe Pic 1140x640.jpeg Freeman Mbowe

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema haikuwa kazi nyepesi kufikia makubaliano ambayo yametangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba sasa mkwamo wa mchakato wa Katiba mpya utafufuliwa bila kuhodhiwa na chama chochote.

Amesema katika kipindi cha miezi saba ambayo ilikuwa ya ubishani mkubwa, wamefanikiwa kuirejesha CCM kwenye reli kwamba suala la Katiba ni la sasa na lazima lijadiliwe.

Mbowe ametoa kauli hiyo jana tarehe 3 Januari, 2023 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais Samia dhidi ya viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live