Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe: Wenye ushahidi kuwa nimenunuliwa na CCM wajitokeze

Mbowe Mdkd Mbowe: Wenye ushahidi kuwa nimenunuliwa na CCM wajitokeze

Sat, 21 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumamosi amesema kashfa ya kutuhumiwa kuwa amekula rushwa au amelamba asali ili kushiriki maridhiano ya kitaifa na CCM ni mojawapo ya kashfa mbaya zilizopitiliza na kushusha heshima yake kwa jamii katika kipindi cha miaka 30 aliyoitumikia Chadema.

Pia ametoa wito kwa mwanachama au mtu yeyote mwenye ushahidi kwamba amechukua senti tano ya CCM ili ashiriki maridhiano hayo ya kitaifa ajitokeze.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Amesema baadhi ya Wana-Chadema walijengewa hofu kwamba mwenyekiti wao ameuzwa kashfa ambayo ni mbaya katika kipindi chote cha miaka 30 kwenye utumishi waka Chadema.

“Anasimama kiongozi wa chama changu anasema Mbowe amepewa asali! nimepoteza mabilioni ya fedha kwenye chama hiki… nimeitesa familia, wanakuja wenzangu wanaotakiwa kuniunga mkono wanasema nimekula rushwa?

“Kwangu ni insult (kashfa) iliyopitiliza, yeyote mwenye ushahidi kwamba Mbowe nimekula senti tano ya mtu asimame aseme… kwa sababu mnaua heshima yangu.

“Mambo ya kuumizana, kudhalilishana siwezi kuyakubali, lakini leo tukubaliane, tusamehe ya nyuma tuende mbele na kwa hilo niko tayari,” amesema Mbowe.

Amesema jambo hilo limemuumiza sio yeye pekee bali pia,watoto wake na mke wake kwa sababu wanajua amepoteza mabilioni mangapi lakini anatokea kiongozi wa Chadema anasema amekula asali na kuaminisha umma.

“Kwa namna amabvyo viongozi wangu wameteswa na kuumiwa upande wa pili wana haki ya kuwa na hisia hizo. Lakini niwaombe viongozi wangu tuna wajibu mkubwa katika nchi yetu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live