Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe: Wanawatoza kodi wanakwenda kununua magari ya mil 500

Mbowe V8 Freeman Mbowe

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.

Kauli za Mbowe;

“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga. Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.

“Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.

“Lakini kwa kuwa kuna pesa ya wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja. Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?

“Magari mapya nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka. Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.

“Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki. Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe,” amesema Mbowe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live