Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe: Wabunge 19 ni ulaghai..!

Mbowepic Siasa Leo Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikel Mbowe amezungumzia sakata la wabunge 19 waliovuliwa uanachama mara baada ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kukubali uteuzi wa ubunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo Machi 8, 2022 jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema kuwa wabunge hao walishavuliwa uanachama hivyo kinachoendelea hivi sasa ni ulaghai wa kisiasa.

Akinukuu kauli ya Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson aliyotoa mapema mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo kuwa kinachosubuliwa na Bunge ni barua ya kuwavua uanachama wabunge hao ambayo kimsingi inapaswa kutoka CHADEMA, Mbowe amesema kuwa kauli hiyo ni ya ulaghai kwani tayari taarifa za kuwavua uanachama zilishawasilishwa Bungeni.

"Kauli ya Tulia ni ulaghai anajua kuwa wale wabunge wameshafukuzwa kwenye chama chetu"

"Baraza Kuu lilishapanga kukutana kama kuna rufaa tutaiona tukikutana, naomba muelewe kuwa tunapokataa wabunge 19 tunakataa uvunjwaji wa sheria za nchi"

"CHADEMA haijawahi kuteua wabunge 19 ieleweke hivyo" Amesema Mbowe.

Aidha Mbowe amesisitiza kuwa kukutana kwake na Rais Samia kunatoa dira njema ya kisiasa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live