Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe, Lisu wagawana mikoa maadamanao Chadema

Chadema 841598 Mbowe, Lisu wagawana mikoa maadamanao Chadema

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeweka hadharani ratiba ya kufanyika kwa maandamano nchi nzima huku mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti Bara, Tundu Lissu wakigawana mikoa kuyaongoza.

Maandamano hayo ni matokeo ya mkutano wao uliofanyika Machi mwaka huu mkoani Mtwara ambako chama hicho kilikuja na Azimio la Mtwara lililolenga kufanya maandamano kwenye mikoa yote kuanzia Aprili 22 hadi Aprili 30.

Agenda za kufanyika kwa maandaano hayo ni katika kufikisha kilio cha uwepo maisha magumu kwa wananchi, kuendelea kusisitiza madai ya Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ambayo imeshaanza kutumika.

Pia, maandamano hayo, yanalenga kupaza sauti ya namna gani nchi inaweza kukabiliana na majanga ikiwamo mafuriko ambayo yameikumba mikoa mbalimbali kwa sasa kutokana na vua zinzoendeea kunyesha nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 18,2024, kuhusu maandalizi ya maandamano hayo yalipofikia hadi sasa, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema baada ya tangazo hilo la Azimio la Mtwara, maandalizi yanaendelea kufanyika na kama chama baada ya kufanya tathimini ya mambo mbalimbali ikiwamo ya hali ya hewa na kuamua kuyagawa kwa awamu mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live