Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia kupinga mchakato wa kumpata spika mahakamani

Mbatiapic Data Mbatia kupinga mchakato wa kumpata spika mahakamani

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (kulia) akiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 21,2022 kwa ajili ya kufungua kesi ya kupinga mchakato wa uteuzi mgombea uspika wa Bunge.

Jana Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imetangaza jina la pekee la Dk Tulia Ackson kuwa mgombea wa kiti cha Spika kilichoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuluzu nafasi hiyo Januari 6, 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 20, 2022 kwenye ukumbi wa White House Dodoma, Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu imepitisha jina moja la Dk Akson kati ya majina 70 ya makada wa CCM waliochukua na kurejesha fomu.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (kulia) akiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 21,2022 kwa ajili ya kufungua kesi ya kupinga mchakato wa uteuzi mgombea uspika wa Bunge.Picha na Michael Matemanga

Utaratibu wa CCM ni kupeleka majina yasiyozidi matatu kwenye kamati ya wabunge. Wanaweza kupeleka moja au mawili au matatu.

Advertisement Dk Tulia anakuwa mwanamke wa pili kuwa Spika kama atachaguliwa na wabunge.

Mbali na CCM, chama cha upinzani cha Alliance for Democratic Change (ADC) nacho kimefungua mchakato huo na mwanachama wake, Maimuna Kassim amekuwa wa kwanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa nafasi ya Spika.

Tutakuletea kitakachojili mahakamani hapo hivi punde

Chanzo: www.tanzaniaweb.live