Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia atangaza safu ya uongozi NCCR-Mageuzi

Video Archive
Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha (NCCR- Mageuzi), James Mbatia ametangaza safu mpya ya viongozi wa juu akiwamo katibu mkuu wa  chama hicho, Elizaberth Mhagama.

Mhagama na viongozi wengine walichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho ulioanza Jumamosi Julai 27, 2019 jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Katika mkutano huo ulioendelea hadi jana Jumapili,  wajumbe wa mkutano huo walimchagua Mbatia kuwa mwenyekiti wa chama hicho, atakayeongoza kwa miaka mitano ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 29, 2019 Dar es Salaam, Mbatia amewataja manaibu makatibu wakuu waliochaguliwa ni Mussa Kombo Mussa (Zanzibar) na Rehema Kahangwa (Bara), wakati makamu wenyeviti ni Haji Ambari Hamis (Zanzibar) na Angelina Muthakiwa (Bara).

"Hii ndio safu ya viongozi wakuu sita ikiongozwa na mimi, uchaguzi ulikuwa huru na haki, tulimaliza jana usiku. Kwenye safu yetu ya uongozi tumejaribu kuzingatia usawa wa jinsia, " amesema Mbatia.

Chanzo: mwananchi.co.tz