Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia asisitiza Tume huru ya uchaguzi

98554 Mbatia2+pic Mbatia asisitiza Tume huru ya uchaguzi

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia amesema msimamo wa chama hicho tangu kilipoanzishwa mwaka 1991 ni kuwa na Katiba mpya ambayo ndani yake kuna Tume huru ya uchaguzi.

Akizungumza leo Jumanne, Machi 10 katika mahojiano na MCL Digital, Mbatia amesema suala la Tume huru ya uchaguzi lilizungumziwa na Tume ya Jaji (Francis), Tume ya Jaji Robert Kisanga na Tume ya Jaji, Joseph Warioba.

“Sisi NCCR Mageuzi, tangu kuasisiwa kwetu mwaka 1991 ndiyo tulianzisha National Committee for Constitution Reform. Tunazungumzia Katiba mpya yenye kufuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na Tume ya uchaguzi ni mtoto wa Katiba mpya,” amesema Mbatia.

“Sisi mpaka leo hii, msimamo wetu bado ni wa kuwa na Katiba mpya inayotokana na umma. Tuwe na makubnaliano ya kmitaifa, namna gani tuendeshe chaguzi zetu tukiwa na Tume inayokubalika na pande zote.”

 

 

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz