Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia ashauri vyama kusitisha mikutano ya hadhara

99322 Mbatia+pia Mbatia ashauri vyama kusitisha mikutano ya hadhara

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ameshauri vyama vya siasa nchini Tanzania kusitisha mipango ya kuendesha mikutano ya hadhara ili kupunguza tishio la kusambaa virusi vya corona (COVID-19). "Kuhusu mikusanyiko, hili ni suala la utaifa, mikusanyiko isiyokuwa na kinga, haijalishi watu 500, watu 200 inabidi tuchukue tafadhali sana," amesema Mbatia alipoulizwa kuhusu baadhi ya vyama vinavyotarajia kuanza mikutano ya hadhara hapo baadaye katikati ya janga hilo. Mbatia ameshauri Serikali kuhakikisha inatoa mwongozo na taarifa mara kwa mara kuhusu hali ya ugonjwa huo pamoja na kuongeza elimu ya uraia kwa raia wanaoendelea kukusanyika. Mbatia ametoa ushauri huo leo Jumanne Machi 17, 2020 jijini Dar es salaam ikiwa ni siku moja baada ya Wizara ya Afya kutangaza rasmi kuingia kwa ugonjwa huo nchini. Mbatia ambaye ni mbunge wa Vunjo amesema tayari ameanza kuchukua tahadhatri hiyo baada ya kisitisha ziara yake Machi 21, mwaka huu katika kata 16 za jimbo hilo.  "Nilitakiwa kuanza ziara hiyo na tayari maandalizi yote yalishakamilika, lakini nimesitisha kwa sababu ya janga hili, kwa hiyo tuchukue tafadhari sana,"amesema Mbatia. Amesema hakuna haja ya kusubiri madhara zaidi katika maambukizi ya virusi hivyo badala yake kila Mtanzania azingatie maelekezo ya kitaalam.

Chanzo: mwananchi.co.tz