Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia asema hawezi kusaliti Ukawa

98548 Mbatia2+pic Mbatia asema hawezi kusaliti Ukawa

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia amesema hawezi kuvisaliti vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 licha ya kukiri  umoja huo kukiathiri chama hicho.

Ukawa iliundwa mwaka 2014 na CUF, NLD, NCCR-Mageuzi na Chadema ilitoa upinzani mkali katika uchaguzi mwaka 2015 hasa baada ya kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi za udiwani, ubunge na urais.

Mbatia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 10, 2020 alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Commucations Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na kumiliki chaneli ya MCL Digital.

Mbatia ambaye ni mbunge wa Vunjo amesema madai ya usaliti ni ya hisia tu.

“Nimezungumzia suala la hisia, wewe unahisi hivyo, mna uhakika hayo maneno niliyasema Mbeya? (katika ziara yake ya siku tatu)? Nilichosema siku ile, sisi tulipoingia kwenye ushirikiano wa vyama tulikuwa na wabunge wa kuchaguliwa wanne, mmoja wa kuteuliwa na mmoja wa Afrika Mashariki tulikuwa sita.”

“Baadaye kwenye ushirikiano tukaathirika tukabaki na Mbunge mmoja. Nikasema wanaponitukana ni nani aliye host Ukawa? Lakini nikasema wasituchokoze zaidi yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Sasa usaliti umetoka wapi,” amesema Mbatia.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Huku akikumbusha chama hicho kukiwekea pingamizi CUF kwenye uchaguzi wa marudio wa mwaka 2002, Mbatia amesema ile ilikuwa ni haki yao kama chama cha siasa.

“Kwamba Mbatia ameweka pingamizi Pemba. Hebu soma sheria ya uchaguzi, kama kiongozi wa chama anaweza kuweka pingamizi dhidi ya mgombea wengine,” amesema.

Amefafanua aliyekuwa mkuu wa kitengo cha sheria cha chama hicho ndio aliyesimamia suala hilo.

“Walikaa kule wakawekeana pingamizi na ni haki ya kila chama kuwekeana pingamizi haikuwa na hiana yoyote. Mkuki ukawa mtamu kwa nguruwe, mtamu kwa binadamu.”

 “Mwenye kadi namba moja ya NCCR Mageuzi ni Mabere Marando yuko chama kingine, umeshawahi kusikia mimi nakigombana na chama kingine? Anthony Komu (Mbunge Moshi Vijijini-Chadema) na Joseph Selasini (Rombo-Chadema)  wamekwenda vyama vingine. Lakini hata wakati wa kampeni za uchaguzi nilikwenda nikawapigia kampeni,” amesema Mbatia.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz