Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbatia aonyesha ugumu wa vyama vya upinzani Tanzania kuungana

98551 Mbatia1+pic Mbatia aonyesha ugumu wa vyama vya upinzani Tanzania kuungana

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameonyesha mazingira magumu ya vyama vya upinzani nchini Tanzania kuungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, akisema marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019, ni lazima umoja huo usajiliwe.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, vyama vinne vya upinzani (Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na NLD) viliungana kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuleta ushindani mkali kwa CCM.

Akizungumza leo Jumanne Machi 10, 2020 katika ofisi ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti zilizopo Tabata Relini, Mbatia ambaye amevilalamikia vyombo vya habari kwa kuchochea migogoro ya vyama vya siasa, amesema kuna tatizo la kutoaminiana ndani ya vyama hivyo.

“Sisi sio tawi la chama kingine. Kila chama kina usajili wake na kwa mujibu wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa yaliyofanyika Januari 29, 2019 kule Dodoma, tukiwa na ushirika wa sasa lazima usajiliwe, ili baada ya uchaguzi utekelezeke,” amesema Mbatia.

Huku akitoa mfano wa uchaguzi wa nchi ya Uholanzi wa mwaka 2002, amesema vyama vya siasa vilishindwa kuunda Serikali kwa miezi sita kwa sababu ya kutoaminiana.

“Mgombea mmoja akamwambia mwenzake, wewe sikuamini, akaendelea kusema wewe ni mwongo. Baada ya uchaguzi hakuna chama kilichopata asilimia 50, sasa yule mmoja akamwomba mwenzake washirikiane.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Yule mwenzake akasema wewe umesema mimi ni mwongo tutakaaje meza moja tuzungumze? Sasa sembuse wakati huu ni mambo gani yanayoendelea,” amesema.

Kuhusu kada wa Chadema aliyehamia chama hicho, Edward Simbeye, mbunge huyo wa Vunjo amekanusha kumruhusu achafue vyama vingine.

“Kwa kauli yangu sikuwahi kumwambia Simbeye asimame jukwaa nililoko mimi kushambulia vyama vingine. Alikuwa amezungumza huko alikotoka, lakini siku alipopokelewa NCCR Mageuzi nilimwambia yaliyokuwa huko uyaache huko uzingatie itikadi yetu ya utu,” amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz